Wednesday, February 12, 2014

MASTAA WA KIKE WALIOONGOZA KWA SKENDO BONGO 2013 NDIO HAWAA

KATIKA ulimwengu wa mastaa kuna ambao wamekuwa wakitikisa kwa skendo mbalimbali kwa mwaka 2013 ambazo ziliwachefua mashabiki wao, Ijumaa Wikienda linakupa Top 10 ya skendo hizo.
AGNES GERALD ‘MASOGANGE’
Video Queen huyo alitikisa mwaka 2013 kwa skendo ya kukamatwa na dawa za kulevya huko Afrika Kusini na kuwekwa rumande kwa siku kadhaa.
Baadaye alifikishwa mahakamani ambapo iligundulika kuwa mzigo aliokuwa amebeba siyo dawa za kulevya ila ni unga unaotumika kama dawa za binadamu na kesi ikaishia hapo.
Pia Masongange alikuwa kinara wa kupiga picha za nusu utupu ambazo alizitundika mtandaoni na kugeuka gumzo kubwa.
WEMA SEPETU
Wema alitikisa kwa ishu ya kurudiana na mwanamuziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ikiwa ni baada ya kukutana nchini China na kupiga picha za kimahaba, hali iliyozua gumzo kila kona na mitandaoni.
Wema alirudiana na Diamond huku akijua kwamba mwanamuziki huyo alikuwa na mpenzi mwingine ambaye ni mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Ukiachilia mbali misala midogomidogo, Wema alitikisa na ile kesi yake ya kumtandika makofi meneja wa hoteli ambapo alisota mahakani hadi alipohukumiwa akalipa faini ya Sh. laki moja.
JACQUELINE WOLPER
Skendo iliyotikisa kwa mwanadada Wolper ni ile ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Ramadhan Mtoro ‘Dallas’ ambayo ilitokea tangu mwaka jana akavuka nayo mpaka mwaka huu.
Pia alitikisa kwa ishu ya kupigania nyumba ya kupanga na Baby Madaha. Baby alidai aliilipia nyumba hiyo Sh. milioni milioni 3.6 na kufanya usafi kwa ajili ya kuhamia lakini siku ya kuhamia alimkuta Wolper ameshahamia na kupanga vitu vyake hali ambayo ilizua mtafaruku kwa wawili hao na kuwa na bifu kali hadi leo.
BABY MADAHA

Mwaka 2013 alitikisa kwa ishu ya kugombea nyumba ya kupanga na Wolper.
Baada ya hapo alitikisa na skendo ya kumuiba mume wa mtu ambaye pia ni meneja wake, raia wa Kenya, Joe Kairuki ambaye yupo naye hadi sasa.

JACQUELINE PATRICK
Mwaka 2013 alitikisa kwa skendo ya kuachana na mumewe, Abdulatif Fundikira ambaye ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu na alipewa talaka mahakamani kabla ya kudaiwa kutoka na msanii Jux.

JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Yeye alitikisa kwa skendo ya kunasa kwenye mtego wa kujiuza ambapo alinaswa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na Global Publishers katika hoteli moja iliyopo Ubungo Dar, baada ya kuelewana na mwanaume aliyekutwa naye kwamba atamlipa kwa dola.
Siku chache baada ya kunaswa na mtego huo Jack Chuz aliolewa na Gadna Dibibi ambaye naye alidaiwa kuwa ni mume wa mtu.
LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
Ikiwa ni siku chache tangu Jack Chuz kunaswa na mtego wa OFM, Aunty Lulu naye aliingia kwenye mtego huo ambapo alinaswa katika hoteli moja iliyopo Sinza, Dar.
KAJALA MASANJA
Mwaka 2013 haukuwa mzuri kwa upande wake kwani aliswekwa jela kwa kosa la utakatishaji wa fedha haramu uliofanywa na mumewe, Faraji Agustino.
Kajala alihukumiwa kwenda jela miaka mitano lakini Wema Sepetu akamlipia faini ya Sh. milioni 13.
Baada ya kutoka gerezani, aliripotiwa kutoka kimapenzi na Petit Man huku akiwa bado ni mke wa mtu.

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’
Yeye alipamba kwenye vyombo vya habari kutokana na skendo yao ya kumgombea msanii mwenzao, Vincent Kigosi ‘Ray’ ambapo alifikia hatua ya kupigana na Chuchu Hans ambaye alidaiwa kuingilia penzi hilo.
CHUCHU HANS
Mwaka 2013, Chuchu alitikisa kwa skendo ya kudaiwa kutoka na mpenzi wa Ruth Suka ‘Mainda’, Ray hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa baina yake na Mainda pamoja na Johari ambaye alimpiga ikiwa ni baada ya tetesi kuzagaa kuwa wawili hao walifumaniwa.
 

No comments:

Post a Comment