Mariam Ismail
Mastaa
wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na
uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja kabisa. wiki kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya mtandao huu kwa kusema " Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena
wanaishi pamoja kabisa, fuatilieni mtajua". Baada ya habari hizo
ilibidi Swahiliworldplanet kuwatafuta mastaa hao, wa kwanza kutafutwa
akiwa Irene Uwoya lakini namba yake ya simu kwa takribani wiki 2 ilikuwa
haipatikani na hata jana alipotumiwa ujumbe kupitia namba yake nyingine
hakujibu.
Baada ya hapo
ilibidi kumtafuta Mariam Ismail ambaye wamecheza filamu nyingi na Irene
Uwoya kama vile Sobbing Sound, Omega Confusion, The Return Of Omega na
Apple, Hata hivyo Mariam anafanya vizuri katika filamu alionekana kuwa
busy na kuchelewa kujibu ujumbe wa madai ya kusagana na Uwoya lakini
jana star huyo aliyejipatia umaarufu kwa kuuvaa vizuri uhusika katika
filamu zake alitoa ushirikiano mzuri kwa kujibu madai hayo akidai sio
kweli ila yeye na Uwoya ni marafiki wa karibu sana na wanasaidiana
katika shida na raha ndiyo maana baadhi ya watu wameshaanza kusema
vibaya...
"Nadhani mimi ndio
mtu wa kwanza kupiga vita upumbavu kama huo... mimi ni mwanamke ambae
nimeumbwa kikamilifu.. sina kasoro yoyote ya kunifanya niwe na mwanamke
mwenzangu....hao wanaofanya upumbavu huo nadhani wana vijikasoro kwenye
mili yao.... Irene Uwoya ni rafiki yangu sana tena urafiki wetu sio wa
leo wala kesho... ni marafiki wa kushibana kabisa... nikoseapo huwa
ananikosoa na yeye akoseapo huwa namkosoa....sometimes huwa tunagombana
na kupatana vitu ambavyo ni vya kawaida katika maisha." alisema Mariam
ambaye hajawahi kukumbwa na skendo yoyote ile kabla.
Mariam ambaye kipaji chake cha filamu hujionyesha waziwazi alimalizia
kwa kusema "Irene ananiheshimu sana na mimi humuheshimu sana Irene,
imefikia hatua ya mimi na yeye tukakaa chini na kupanga tuishi wote kitu
ambacho sioni tatizo na hilo. Ingekua ni chumba kimoja hapo sawa...
lakini ni nyumba kubwa yenye kujitosheleza...kila mtu na room
yake...tunaishi kwa amani na kwa kushirikiana penye tatizo hulitatua
wenyewe bila kumshirikisha mtu. Ukimya wetu na kupatana kwetu
kusiwafanye watu kuanza kuhisi upumbavu juu yetu... natumai ujumbe wangu
utawafikia mashabiki wangu wote. Asante. In god I trust." |
No comments:
Post a Comment