Na Jelard Lucas
MISS Tanzania 2011, Salha Israel ameweka
bayana bila ya woga wowote kuwa, kwenye pochi yake hakaukiwi na mipira
ya kiume ‘kondom’, Amani linakupa kila kitu kinagaubaga.
Salha alisema hayo, juzi Jumanne katika
mahojiano maalum, chumba cha habari cha Magazeti Pendwa Bongo, Global
Publishers, Bamaga – Mwenge jijini Dar es Salaam.
HABARI KAMILI
Katika mahojiano hayo, Salha aliwekwa
mtu kati ambapo alifafanua ishu hiyo pamoja na mambo mengine ndani na
nje ya urembo, bila kusahau tasnia ya sinema ambayo kwa sasa ameingia
kwa miguu miwili.
Swali la msingi lililozaa jibu hilo ni
pale alipoulizwa kama aliwahi kutoa mimba tangu alipoanza kuelea kwenye
bahari ya mapenzi, ambapo alikana kisha akafafanua: “Mimba! Weeeee....
hapana. Sijawahi kupata wala kutoa mimba.”
Akaongeza: “Mimi natumia kondom bwana, mimba itaingia wapi hapa!”
AMANI: Kama ukienda kwa jamaa na akawa hana kondom unafanyaje?
SALHA: Na kwa nini asiwe nayo? Lakini
siyo tatizo sana, ndiyo maana mimi huwa nakuwa nazo kwenye pochi muda
wote. Nikijua nakwenda kwa jamaa, basi zinakuwa tayari.
Sitaki kisingizio, kama atakuwa nazo
fine (sawa) but (lakini) akiwa hana natoa zangu. Unajua mimi ndiye
nitakayeingia kwenye matatizo ndiyo maana nakuwa makini mwenyewe.
AMANI: Kwa hiyo hata sasa hivi hapo unazo kondom kwenye pochi yako?
SALHA: (Anacheka) Hapana, hapana... kwa
sasa sina na hii ni kwa sababu sina mtu muda huu ila nikiwa naye huwa
siachi kuzibeba muda wote.
No comments:
Post a Comment